Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kinondoni Mhe.Iddi Azzan akiwahutubia Wananchi wa Mwananyamala katika mkutano wake wa kamepeni uliofanyika katika viwanja vya galilaya. aliwataka Wananchi kukipa kura Chama Cha Mapinduzi ili kuwapatia Huduma zilizobora. akitoa mfano kwa sasa mpango unaoendelea kwa kila kata ni kuhakikisha inajengwa Zahanati ambayo itakuwa inatoa huduma za kiafya ili kurahisisha na kuipungumzia mzigo Hospitali ya Mwananyamal.
Pia aliwaeleza kuhusiana na Suala la Maji kuwa Serikali iko katika harakati za kuhakikisha wananchi wanapata maji ikiwa wanashirikiana na wataalamu kutoka nje ambao teyari wameshaanza kufanya kazi hizo ili kuhakikisha Watanzania wanaondokana na shida hiyo.
Mwisho aliwaomba Wananchi wa kata hiyo kumchagua Mhe.Jakaya kikwete katika nafasi ya Urais, Udiwani katika kata hiyo Ndugu Songoro Mnyonge na katika nafasi ya Ubunge wa Jimbo hilo la Kinondoni yeye mwenyewe Mhe.Iddi Azza.. "KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI"
Mhe.Iddi Azzan akimnadi Mgombea Udiwani wa kata ya Mwananyamala Ndugu Songoro Mnyonge ili aweze kushirikiana nae katika kazi za kiserekali.
Bizainab Mwinyi ajiengua katika Chama Cha Wananchi CUF baada ya kuzikubali sera za Chama cha Mapinduzi CCM, bibi huyo alirejesha kadi yake ya CUF kwa Mhe.Iddi Azzan wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kata ya Mwananyamala.
Bizainabu akikabiziwa mingaro ya CCM.
Mhe.Iddi Azzan akimtambulisha Chipukizi Mohammed.
Ndugu Rashid Kimbanga akiburudisha Wananchi kwa nyimbo yake ya CCM.
Mhe.Iddi Azzan na Ndugu Songoro wakiwa meza kuu wanaangalia Wasanii wanavo burudisha
"Baraka ya nyumba watoto" Watoto waikubali CCM
Wananchi wakisikiliza Sera za Wagombea.
No comments:
Post a Comment