Sunday, October 31, 2010

KILELE CHA KAMPENI CHAFIKIA MWISHO HUKU MHE.DK JAKAYA KIKWETE AKIFUNGA KAMPENI ZAKE VIWANJA VYA JANGWANI.

JK akipanda jukwaani kwa mbwembwe huku akicheza nyimbo ya bongo flava ya kizazi kipya kabla ya kuhutubia mkutano wake wa mwisho wa kampeni viwanja vya jangwani jijini Dar jana.
JK akimpa mkono mke wake Mama Salma Kikwete baada ya kuhutubia huku mgombea mwenza Dk. Mohamed Ghalib Bilal, Katibu Mkuu wa CCM Mh. Yusuf Makamba, Makamu wa CCM (Bara) Mh. Pius Msekwa na marais wastaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Mh. Benjamin Mkapa pamoja na Waziri Mkuu mstaafu Mh. Joseph Sinde Warioba wakisubiri zamu zao
JK akisalimiana na mgombea mwenza wake Dk. Mohamed Gharib Bilal wakati akishuka jukwaani baada ya kumaliza kutoa salamu kwenye hafla ya kufunga mikutano ya kampeni kwa CCM, iliyofanyika kwenye viwanja wa Jangwani jioni ya Jana.
Dk. Mohamed Gharib Bilal akisalimiana na Rais Mstaaafu wa awamu ya tatu,Mh. Benjamin Mkapa na rais Mstaafu wa awamu ya pili,Mh. Ali Hassan Mwinyi wakati alipomaliza kutoa salamu zake kwa wapenzi na wanachama wa CCM waliofurika leo katika viwanja vya Jangwani jijini Dar wakati wa hafla ya kufunga mikutano ya kampeni.
Rais Benjamin Mkapa akihutubia
Meza kuu ikimpongeza rais Mstaafu Mh. Benjamin Mkapa kwa hotuba iliyotukuka
Rais Mstaafu Mh. Benjamin Mkapa akiwa na mawaziri wakuu wastaafu Dk. Salim Ahmed Salim, Mh. Joseph Sinde Warioba na Mgombea mwenza wa JK , Dk. Mohamed Ghalib Bilal
Mheshima Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wananchi wakati alipowasili kwenye viwanja vya Jangwani kwa ajili ya kufunga mikutano ya kampeni kwa CCM.
Mheshimiwa Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mjumbe wa Halmashauri kuu kwa Mkoa wa 
Dar es Salaam, Asha Baraka, wakati akiingia kwenye viwanja vya Jangwani.
Dk.Jakaya Kikwete akipokelewa kwa nderemo alipowasili Jangwani
Nyomi haikuwa ya kawaida Jangwani.
Sehemu ya nyomi ya CCM Jangwano leo


No comments:

Post a Comment