Thursday, October 14, 2010

WAZEE WA KATA YA KIGOGO NA MH.IDD AZZAN WAMUENZI MZEE NYERERE.

Hayati Baba  wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Mh.Iddi Azzan akiwahutubia wazee akisema kuwa Mwalimu Nyerere ataendelea kukumbukwa kwa kuwa aliijenga Tanzania katika misingi imara pamoja na kuondoa baguzi zote, Zarangi, Ukabila, Kidini.

Leo ni Nyerere Day watanzania tunamkubuka baba wa taifa Mwl J.K.Nyerere ambaye tangu atutoke mwaka 1999 ni miaka 11. Watanzania tunapaswa kumuenzi mwalimu kwa mengi lakini kuu ni ile falsafa yake ya umoja ambayo ilimpelekea kuunganisha Tanganyika na Zanzibar hivyo hatuna budi kuuenzi muungano wetu. Mwalimu Nyerere anaheshimiwa na watanzania wengi kwa uadilifu na moyo wake wa kutumikia kuliko kutumikiwa.....Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi.
Wakiwa wamesimama kwa muda wa dk 1 kumuombea baba wa Taifa Hayati Mwl.J.K.Nyerere.
Wazee wa kata ya kigogo wakiwa katika mkutano wa kumuenzi baba wa taifa Mwalimu Julius kambarage nyerere.
Wazee wakisikiliza kwa makini historia fupi ya Mwl.Nyerere iliyokuwa ikitolewa na Mh.Iddi Azzan.

No comments:

Post a Comment