Thursday, October 28, 2010

MHE.ALI HASSAN MWINYI AMNADI MBUNGE WA KINONDONI.

Mhe.Ali Hassan Mwinyi Rais Mstaafu akisiitiza kwa Wananchi kukipigia kura Chama Cha Mapinduzi na Kumchagua Mgombea Urais Mhe.Jakaya Kikwete Gari kubwa, Mbunge na Madiwani katika Mkutano wa kampeni uliofanyika Magomeni makuti viwanja vya CCM. 
Rais Mstaafu Mhe.Ali Hassan Mwinyi akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kinondoni Mhe.Iddi Azzan katika kata ya Mgomeni(Uwanja wa Nyumbani) ndiko anakotokea Mhe.Iddi Azzan.
Mgomba Ubunge wa Jimbo la Kinondoni Mhe.Iddi Azzan akiwahutubia Wananchi na kuwaeleza sera zake ikiwa ni kuboresha Vituo vya Afya,barabara,Elimu,Maji na kujenga Zahanati kwa kila kata. Pia akiwaomba Wananchi Kukipigia kura Chama Cha Mapinduzi kuanzia Urais Mhe.Jakaya kikwete, Mbunge kwa Jimbo la Kinondoni yeye mwenyewe Mhe.Iddi Azzan na Madiwani wote wa kata zote za Jimbo hilo.
Rais mstaafu Mhe.Ali Hassan Mwinyi akiwani Wagombea Udiwani kuanzia (Kulia) Mgonja kata ya Ndugumbi, Husna Kata ya Kinondoni na Mwisho (kushoto) Bulembo kata ya Magomeni, akiwaomba Wananchi wa wachague ili waweze kushirikia na Mbunge na Rais.
Mhe.Iddi Azzan akimpa mkono Rais Mstaafu Mhe.Ali Hassan Mwinyi baada ya kumaliza kuhutubia Wananchi waliohudhuria Mkutano huo wa kampeni.
Wananchi wakimsikiliza kwa makini Mgombea ubunge Mhe.Iddi Azzan.

 Mtu nyomiiii.
Wananchi wakiwa wametulia kusikiliza yaliyo anadaliwa.
 Waigizaji wa Mizengwe wakiburudisha...!
 Chipukizi Mohammed akiwaburudisha Wananchi kwa Sera zake za kukiombea kura Chama Cha Mapinduzi
Kikundi cha wa kina dada kikiburudisha jukwaani kwa nyimbo ya alajiiiii.
No comments:

Post a Comment